Surah 105 · 5 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Fil in Swahili

In English with tafsir

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

105:1

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu

105:2

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٍ

Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu

105:3

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana

105:4

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ

ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu

105:5

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٍ مَّأۡكُولِۭ

Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.