Surah 102 · 8 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr
Surah At-Takathur in Swahili
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ
Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu
حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ
Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo
كـَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu
ثُمَّ كـَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera
كـَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ
Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu
ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ
Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo
Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.