Surah 85 · 22 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr

Surah Al-Buruj in Swahili

In English with tafsir

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

85:1

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi

85:2

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ

Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya

85:3

وَشَاهِدٍ وَمَشۡهُودٍ

Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Anachokitaka. Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina

85:4

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ

Wamelaaniwa waliofukua chini ya ardhi shimo kubwa ili kuwatesa Waumini

85:5

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ

Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi

85:6

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٌ

Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo

85:7

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٌ

Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini

85:8

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake vitendo Vyake na sifa Zake

85:9

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ شَهِيدٌ

Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake

85:10

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, kisha wasitubie, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma

85:11

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٌ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ

Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari yapita mito. Huko ni kufaulu kukubwa

85:12

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Hakika malipizo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito

85:13

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ

Ndiye Yeye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha

85:14

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ

Ndiye Yeye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaoikurubisha kwake

85:15

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ

Mwenye Arshi tukufu

85:16

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

Mfanya Alitakalo: hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe

85:17

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ

Je, ewe Mtume, imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletwa, ya

85:18

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ

Firauni na Thamūd, misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo

85:19

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٍ

Bali waliokufuru waendelea kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao

85:20

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ

Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka kwa Ujuzi na Uweza Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qu’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi ndipo wakaikanusha

85:21

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٌ مَّجِيدٌ

Bali hii ni Qur’ani kubwa iliyo tukufu

85:22

فِي لَوۡحٍ مَّحۡفُوظِۭ

iliyomo kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na kubadilishwa wala kupotoshwa

Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.