Surah 84 · 25 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr
Surah Al-Inshiqaq in Swahili
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ
Pindi mbingu itakapopasuka na kudhihiri mawingu katika pasuko zake Siku ya Kiyama
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ
Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ipasuke, na inastahili kufuata amri hiyo
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ
Na ikatii amri ya Mola wake ya kuwa ifanye hivyo, na inastahili kufuata amri hiyo
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحًا فَمُلَٰقِيهِ
Ewe binadamu, wewe unaenda kwa Mwenyezi Mungu na unafanya amali nzuri na mbaya, kisha utakutana na Yeye Siku ya Kiyama. Na huna budi kupata kutoka Kwake malipo mazuri zaidi ya amali yako njema au yanayolingana na amali yako mbaya
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
Yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa mkono wake wa kulia
فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا
naye ni yule aliyemuamini Mola wake, atahesabiwa hesabu pesi
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ
Na yule mwenye kupewa waraka wa amali zake kwa nyuma ya mgongo wake
فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورًا
naye ni yule aliyemkanusha Mwenyezi Mungu, ataita maangamvu na hasara
إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا
Hakika yeye alikuwa kwa watu wake ulimwenguni ni mwenye furaha na majivuno, hafikirii mwisho wake utakuwa namna gani
بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا
Sivyo hivyo! Mwenyezi Mungu Atamrudisha kama alivomuumba na kumlipa kwa amali zake. Kwani Yeye kwake ni Mtambuzi na kwa hali yake ni Mjuzi kuanzia Alipomuumba mpaka kumfufua
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ
Mwenyezi Mungu Ameapa kwa wekundu wa pambizo za mbingu wakati wa kutwa jua
وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ
Na kwa usiku na viunbe tofauti - tofauti vya kutambaa, kuruka na kutembea kwa miguu, uliokusanya
لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ
Mtapitia, enyi watu, miongo mbalimbali na hali tofauti : kutoka kwenye tone la manii, kuptia pande la damu, nofu la nyama hadi kutiwa roho, mpaka kufa na mpaka kufufuliwa. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, afanyapo hilo atakuwa ameingia kwenye ushirikina
فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Ni kitu gani kinachowazuia kumwamini baada ya aya zake kufafanuliwa kwao
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ
Na wana nini wao wanaposomewa Qur’ani hawamsujudii Mwenyezi Mungu wala hawajisalimishi kufuata yaliyokuja ndani yake
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ
Hakika tabia ya waliokufuru ni kuikanusha na kuikataa haki
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi wa ukaidi wao wanaouficha kwenye nyoyo zao hali wao wanajua kuwa yale yaliyoletwa na Qur’ani ni kweli
فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Basi wape bishara, ewe Mtume, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Amewaandalia adhabu yenye uchungu
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ
Lakini wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakatekeleza amri waliyofaradhiwa na Mwenyezi Mungu watakuwa na malipo, Siku ya Akhera, yasiyokatika wala kupungua
Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.