Surah 88 · 26 verses · Abdullah Muhammad Abu Bakr
Surah Al-Ghashiyah in Swahili
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ
Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu
لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ
Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno
لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٍ
Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa
لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٌ
Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ
Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu
وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ
Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi
فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌ
Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao
لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ
Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ
Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake
Translation: Abdullah Muhammad Abu Bakr.